"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Kenyan Booklets

KANISA  LA  KWELI  LA  MUNGU


Chapa ya Kwanza, 2001 (Kiingereza)

Copyright  ©  2001 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
P. O. BOX 328,
Rogue River, OR  97537
U.S.A.



     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.



     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message,
P.O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA,
EAST AFRICA.

AU

Booklets
P.O. BOX 328
ROGUE RIVER, OR  97537
U.S.A.




KANISA  LA  KWELI  LA  MUNGU

     Kwa maelfu ya miaka swali juu ya nani na kipi kinafanya Kanisa la Mungu imeleta mjadala mkubwa. Wengine, wakiwa wamejifunza wenyewe, wamepambanua umuhimu wa ukweli huu. Wakati wengine huenda hawakuelewa, au wamedharau, ukweli kuhusu mada hii. Kupambanua ukweli huu ni kupata uhuru ndani ya Yesu Kristo, lakini kuukanganya ndiyo hatua ya kuwa kifungoni na utumwa wa Shetani. Kwa hiyo mada hii ni ya muhimu sana kwa wafuasi wote wa Mungu ili wachukue muda kujifunza na kufahamu nani na ni kipi hufanya Kanisa la kweli la Mungu.
     Kadiri ambavyo kuna yumkini madhehebu 100 tofauti leo na yote yakidai kuwa Kanisa la kweli la Mungu, na bado yote yanahitilafiana moja baada ya jingine katika imani; Je, haya yote yanaweza kuwa Kanisa la kweli la Mungu? Tutajuaje kwa uhakika? Njia pekee ya kufahamu ni kupata maarifa na hekima; lakini kutoka wapi? Je, tunaweza kutegemea tu maarifa na hekima ya vyanzo vya kidunia? Hapana, kwa sababu tunaweza kuwa maadui wa Mungu (angalia Yakobo 4:4). Je, tunaweza basi kutegemea tu maarifa na hekima kutoka kwa watu wengine? Hapana, kwa sababu kama tutategemea maneno ya watu wengine – wawe ni papa au kasisi, mchungaji [mhudumu] au mzee wa kanisa, guru au mganga, tutalaaniwa (angalia Yer 17:5). Je, tutegemee basi maarifa yetu pekee? Hapana, kwa sababu hayo ni upuzi (angalia 1 Kor 1:19-20, 3:19). Basi ikiwa ni hivyo tutapata wapi maarifa na hekima ambayo yatatusaidia kufahamu nani na kipi hufanya Kanisa la Mungu? Lazima iwe kutoka katika neno la Mungu mwenyewe, na kwa rehema huahidi kutupatia maarifa yote na hekima tunayohitaji kuelewa ukweli wake (angalia Yak 1:5; Yoh 7:17, 14:26). Hekima na maarifa ambavyo hutoka kwa Mungu, kama yanavyopatikana katika neno lililovuviwa, lazima yawe TU msingi wetu na kitu cha kutegemea katika harakati za kuelewa ukweli wa suala hili muhimu.
     “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa 8:20.

     “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” 2 Tim 2:15.

     Lazima tuchunguze na kujifunza neno la Mungu wenyewe ili kujua ni nani na ni nini kimeelezwa kuwa Kanisa la Mungu, na hatutakiwi kuruhusu mtu yeyote kuchukua dhamiri zetu au kufanya kazi ya kujifunza kwa ajili yetu. Na kuwa na hakika kwamba tunapata ufahamu sahihi, lazima turejee tena kwenye ukweli wa msingi kama unavyopatikana katika neno la Mungu lililovuviwa, na hivyo kujenga mwamba imara wa ukweli ambao tunaweza kusimama juu yake.

     Kwa kuwa kuna mamlaka mbili tu ulimwenguni – mamlaka takatifu au ya uovu, na vyanzo viwili pekee vya mafundisho – vya nuru au giza, kwa hiyo neno la Mungu limeorodhesha aina mbili tu za Makanisa – Kanisa safi lenye haki la Mungu (angalia Ufu 12:1-5; Efe 5:27), au sinagogi potofu la Kibabeli (angalia Ufu 2:9, 17:1-6). Kanisa la Mungu limejengwa tu juu ya nuru ya Mungu ya ukweli (angalia 1 Timotheo 3:15), kwa sababu Mungu tu ndiye mwanzilishi wa nuru, wema na ukweli (angalia Mwanzo 1:3-4; Mathayo 19:17; Yakobo 1:17).
     Wakati Kanisa la Shetani limejengwa juu ya uongo, kwa sababu Ibilisi ni mwasisi wa giza lote, makosa na udganganyifu (angalia Isa 14:4-23; Eze 28:15-17; Ufu 12:7-9; Yoh 8:44). Kwa hiyo kama Kanisa lolote linashikilia mchanganyiko wa ukweli na makosa, haliwezi kamwe kuwa Kanisa la Mungu, bali ni sehemu ya sinagogi la Shetani, kwa sababu Kristo na Shetani hawaunganishwi au kuwa na shirika pamoja wakati wowote (angalia Yoh 14:30; 2 Kor 6:15).

     Kanisa la kweli la Mungu lina Kristo pekee kama Kichwa chake na Kiongozi (angalia Efe 1:22, 5:23-24; Kol 1:18). Hivyo, likiwa na Kristo kama Kiongozi wake litafanya tu mambo yale yanayompendeza Mungu (angalia Zab 92:15; Yoh 8:29), na kwa kufanya hivyo milango ya kuzimu haitalishinda kwa sababu hakuna kitu chochote ambacho Ibilisi anaweza kukipata ili akitumie kwa manufaa yake (angalia Yoh 14:30; Mt 16:18). Hivyo, Kanisa la Mungu haliwezi kuanguka na wala halitaanguka, lakini litasimama milele kwa sababu limejengwa juu ya Mwamba usiotikisika wa Milele na Milele – ambao ni Kristo Yesu (angalia Kumb 32:4; 2 Sam 22:32; Zab 18:2; Mt 7:24-25). Wakati ambapo Kanisa ambalo Shetani analitawala litamweka mwanadamu kama kichwa chake na kiongozi (angalia 2 Thes 2:3-4). Hivyo, Kanisa hilo halitatenda mambo yale ambayo humpendenza Mungu, bali litafanya mambo yale yanayowapendeza wanadamu (angalia Mt 16:23). Kanisa hili bila shaka halitasimama, lakini hakika yake litaanguka na kuangamizwa, na wale wote watakaobaki ndani yake, kwa sababu limejengwa juu ya miamba ya mchanga inayobadilikabadilika, isiyo imara, na inayodanganya – ambayo ni ya wanadamu wanaoanguka na hata kufa (angalia Kumb 32:31,37-39; Mt 7:26-27; Ufu 18:2-8).
     Kama ukweli wa Kibiblia hapo juu unavyodhihirisha wazi ni kwamba Kanisa la kweli la Mungu halitelezi hata siku moja kutoka kwenye wema, nuru, na kweli kwa wakati wowote, hata kwa yodi moja tu, na wengi wa watu wa kidini hushindwa kupambanua hili. Hutangaza kwamba utambulisho huu wa Mungu wa Maandiko juu ya Kanisa la kweli la Mungu ni mfinyu na uliobana kwa yeyote kuwa sahihi. Hatimaye, huchemsha fikra kwamba hakujapata kuwapo na dhehebu lolote katika historia yote ya ulimwengu huu ambalo limefanya yale mambo mazuri tu yanayompendeza Mungu kwa nyakati zote. Na kadiri ambavyo hawawezi kufikia tafakari zao kuwa sawa na ukweli wa Maandiko na maarifa haya ya kihistoria, huchanganyikiwa, Maandiko yaliyo hapo juu hupuzwa, na huongozwa kudhani kwamba Kanisa la kweli la Mungu limejengwa na mchanganyiko wa wema na wabaya wakiishi pamoja ndani yake. Lakini hakuhitajiki kuwepo na kuchanganyikiwa, kwa sababu hakuna kujikanganya kati ya Maandiko na ukweli kihistoria kuhusiana na mada hii! Unaweza kusema, hii itafanyikaje? Shida yote iko katika ufahamu wetu wa nani na nini hujenga Kanisa la kweli la Mungu.
     Makutano wamefundishwa kwamba Kanisa la kweli la Mungu limejengwa na jengo, au dhehebu, ambalo limejikita katika ibada ya Mungu. Kwa uelewa huu mawazoni, kuna hitaji la haraka kutafuta dhehebu la kujiunga nalo; lakini ni lipi? Kukiwa na madhehebu 100 au zaidi ya kuchagua, na yote haya yakitangaza kwa ushahidi kwamba ndiyo Kanisa la kweli na pekee la Mungu, kutakuwepo hata kuumwa na mishipa katika kutafakari ni lipi la kweli na linalopasa kuchaguliwa! Lakini kwa kutumia wazo hili, watu wameongozwa kuamini kwamba lazima wawe washiriki wa, au la sivyo kama hawatajiunga na, dhehebu ili kumwabudu Mungu, kuwa sehemu ya Kanisa lake la kweli, na hivyo kuhakikishiwa wokovu wao. Lakini hiki sicho Maandiko yanachofundisha kuhusiana na Kanisa la kweli la Mungu!

     Yesu, katika kuongelea juu yake mwenyewe na Kanisa la kweli la Mungu, alitamka:
     “Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi....Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo...kisha kutakuwapo kundi moja na mchungaji mmoja.” Yoh 10:14-16.

     Awali ya yote, Yesu alisema kuwa Mungu analo “zizi moja” au Kanisa la kweli la Mungu – siy mengi! Kwa hiyo ukweli wa Maandiko hutoa picha sahihi kwamba madhehebu yote kwa pamoja hufanya Kanisa la Mungu. Neno “zizi” hutafsiriwa sawa kama “kundi” (angalia Strong’s Concordance, #4167). Kwa hiyo nani au nini hufanyanyiza ishara hii ya Kanisa la kweli la Mungu – “zizi lake moja” au “kundi moja?” Watu wamefundishwa kwamba zizi moja pekee la kweli la Mungu au Kanisa ni dhehebu – kama Kanisa Katoliki. Lakini kundi moja la Mungu ni dhehebu fulani hasa?
     “Na ninyi, kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.” Eze 34:31.

     Hivyo Kanisa moja la kweli la Mungu, zizi lake moja, kundi lake moja la leo siyo dhehebu – bila kujali jina lao lililotukuka, au jinsi wanavyojishuhudia kwa sauti, kwa sababu Kanisa moja la kweli la Mungu linajengwa na watu. Lazima tuelewe dhana hii muhimu ya ukweli, kwamba Kanisa la Mungu limejengwa na watu na siyo dhehebu, ili wawe huru katika Kristo na siyo kuendelea kubaki katika kifungo na utumwa wa wanadamu!

     Hata katika kipindi cha Kristo vita ya mambo ya kidini ilikuwa inatishia. Wafuasi wa Makanisa mbali mbali walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kupata washiriki na haki ya kujitangaza wenyewe kama Kanisa pekee la kweli na la Mungu. Kila dhehebu lilikuwa likitangaza kwamba ni wao tu walikokuwa na ukweli, na ni katika Kanisa lao tu ndipo Mungu angeabudiwa kikamilifu. Lakini, ni kweli kwamba Kristo alihalalisha imani hiyo? Je, Kristo alichagua dhehebu moja kuwa bora zaidi ya jingine ili watu wake wapate kuabudu humo? Mtu mmoja alimwuliza Yesu moja kwa moja swali hili, na tafadhali soma kwa uangalifu ni jibu gani alimpatia:
     “Yule mwanamke [wa Samaria] akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Baba zetu waliabudu katika mlima huu [hekalu katika mlima Gerizimu], nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudu. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa [ujumbe wa] wokovu watoka [ulikabidhiwa] kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Yoh 4:19-24.

     Kwa hiyo Kanisa la kweli la Mungu halijajengwa na dhehebu hili au dhehebu lile, lakini limejengwa na watu wanaomwabudu Mungu katika roho na kweli. Hivyo basi huhitajiki kutafuta dhehebu lolote ili upate kumwabudu Mungu, lakini unaweza kumwabudu hapo hapo nyumbani kwenu – kama walivyochagua mitume na wafuasi wa Kristo kufanya (angalia Rum 16:5; 1 Kor 16:19; Kol 4:15; Flm 2). Maarifa haya mazuri kwamba Kanisa la Mungu limejengwa na watu na siyo dhehebu lolote ndiyo pekee yatakayokuweka huru katika Yesu, na kukuongoza kwa usahihi kuelewa mada zingine zinazohusiana na Kanisa la Mungu. Ambapo, imani kwamba Kanisa la kweli la Mungu ni dhehebu, itakuacha katika utumwa kwa watu, na kutoelewa mada zingine zinazohusiana na Kanisa la Mungu.

     Bado wengine wanaweza kuwa wangali wana shida katika kuona tofauti kati ya uelewa huu wa aina mbili, kwa hiyo hebu kwa kifupi tuchunguze matukio yafuatayo yanayohusiana na hili kutoka katika hali zote mbili ambazo zitatuwezesha kuonyesha tofauti kati ya mada mbili, na itakuwa wazi kwa nini moja hutuongoza kuwa huru katika Kristo, wakati nyingine inatupeleka katika utumwa kwa mwanadamu.
     Bibllia hufundisha kwamba Mungu anatoa pumziko kwa wale waliochoka (angalia Isa 28:12, 30:15; Yer 6:16). Kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu limeundwa na watu, basi kila mmoja wetu binafsi angetafuta pumziko lake tu kwa kwenda moja kwa moja kwa Yesu (angalia Zab 37:7; Mt 11:28-30), na kama tukichagua kumwacha, basi tunapoteza pumziko letu na wokovu. Ambapo kwa ufahamu kwamba Kanisa la Mungu ni dhehebu, basi tutatafuta pumziko letu kwa kwenda moja kwa moja kwenye dhehebu tu, na kama tukichagua kuliacha dhehebu, ndipo tunaamini kwamba tumeliacha pumziko letu na tumepotea.
     Biblia pia hufundisha kwamba Kanisa la Mungu ni mwili wa Kristo (angalia 1 Kor 12:27; Efe 1:23, 5:30). Kwa hiyo katika kuelewa kwamba Kanisa la kweli la Mungu limejengwa na watu, basi kila mmoja wetu binafsi tunakuwa sehemu ya mwili wa Kristo kwa kujiunga na Kristo mwenyewe na tunabatizwa (angalia Gal 3:27-29; Mt 12:30; Rum 12:5; Mk 16:16). Na kama tungechagua kutoka kwa Kristo, basi tusingekuwa tena sehemu ya mwili au Kanisa na tumepotea. Ambapo kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu ni dhehebu, basi tungekuwa sehemu ya mwili wa Kristo kwa kujiunga na dhehebu kwa njia ya ubatizo. Na kama tungechagua kuhama, au tungefutwa, na dhehebu, basi tungeamini kwamba sisi si sehemu tena ya mwili wa Kristo na tumepotea.
     Biblia hufundisha kwamba watu wa Mungu watapata miili ya kutokufa au uzima wa milele (angalia Rum 2:7). Kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu limejengwa na watu, basi tungepata uzima wa milele kupitia kwa Yesu tu (angalia 1 Tim 1:16-17; 1 Yoh 1:1-2; Yoh 1:1-4, 14:6), na kwa kujiondoa wenyewe kutoka kwa Kristo, hatuna nafasi ya kupata uzima wa milele. Ambapo kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu ni dhehebu, basi tunapata uzima wa milele kwa njia ya dhehebu, na kwa kujitenga wenyewe kutoka kwenye dhehebu tunaamini hatuna nafasi ya uzima wa milele au wokovu.
     Kama unavyoona, matukio haya yote huhusisha suala la wokovu wetu! Biblia hufundisha kwa dhati kwamba inatupasa tuokolewe (angalia 1 Tim 2:3-4). Kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu limejengwa na watu, basi sisi binafsi tungepata wokovu wetu kwa kushikamana moja kwa moja na Yesu Kristo (angalia Yoh 3:17; Isa 45:22; Mdo 2:21, 4:10-12, 15:11, 16:30-31; Rum 5:9-10) na kwa kujitenga wenyewe kutoka kwa Kristo, tumepotea. Ambapo kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu ni dhehebu, basi tunapata wokovu wetu kwa kushikamana wenyewe kwenye dhehebu, na kwa kujitenga wenyewe kutoka kwenye dhehebu, tunaamini tumepotea.

     Sasa hebu na tuweke mawazo yote haya pamoja. Kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu limejengwa na watu, basi sisi binafsi tungepata pumziko letu, kuwa sehemu ya mwili wa Kristo na Kanisa la kweli, kupata uzima wa milele na wokovu, kwa kwenda moja kwa moja kwa, na kushikamana moja kwa moja na, Yesu. Hivyo, macho yetu yanaelekezwa juu, na usikivu wetu unaelekezwa na kulenga kwa Yesu. Huwa mtu [Kristo] tunayetafakari kumpenda, kumsujudia na kumsifu. Yesu huwa yote katika vyote kwetu, maisha yake huwa mada nzuri kwetu inayochukua fikra zetu kutafakari. Ambapo hitaji letu kumpendeza Yeye huchukua nafasi ya kwanza, na mapenzi yake na amri huwa furaha yetu kufuata na kutii. Na kwa kuendelea kumtazama Yesu siku kwa siku, maisha yetu wenyewe na tabia hubadilishwa zaidi na zaidi katika sura yake kamili, na hitaji letu kuwaongoza wengine kujiunga pia na Yesu na kupata wokovu kwake huongezeka kila siku. Lakini kwa kuacha, kujitenga, kujiondoa na kuvunja uhusiano wetu wenyewe kutoka kwa Yesu, basi huwa tena hatuna pumziko; hatuko tena sehemu ya mwili wake au Kanisa la kweli; hatuna tena uhakika wa wokovu au tumaini la uzima wa milele; ambapo ina maana kwamba tumepotea.
     Lakini kwa uelewa kwamba Kanisa la Mungu ni dhehebu, basi tungepata pumziko letu, kuwa sehemu ya mwili wa Kristo na Kanisa la kweli, kupata uzima wetu wa milele na wokovu, kwa kwenda moja kwa moja, na kwa kujishikamanisha moja kwa moja na, dhehebu. Hivyo, macho yetu yanaongozwa chini, na usikivu wetu huelekezwa na kuangalia kwenye dhehebu. Huwa kitu kinachochukua upendo wetu, masujudio na sifa. Dhehebu huwa yote katika vyote, historia yake huwa mada yetu tunayoipenda zaidi kutafakari, na hitaji letu kulipendeza dhehebu huchukua nafasi ya juu. Mapenzi na amri za viongozi wa dhehebu huwa furaha yetu kufuata na kutii. Na kwa kuendelea kulitazama dhehebu, maisha yetu na tabia zetu zinabadilishwa zaidi na zaidi katika sura isiyo kamili inayodhihirishwa, na hitaji letu kuwaongoza wengine kujiunga na sisi katika dhehebu huongezeka zaidi kila siku. Lakini kwa kujiondoa, kujitenga, kutojishikamanisha na kuacha uhusiano wenyewe na dhehebu, basi tunaamini hatutakuwa tena na pumziko; tunaamini sisi siyo tena sehemu ya mwili wa Kristo au Kanisa la kweli; na tunaamini hatuna tena uhakika wa wokovu na tumaini la uzima wa milele; ambapo ina maana kuwa tunaamini tumepotea.
     Matokeo ya hatari kwa wale wanaoamini namna hii, ni kwamba viongozi wa dhehebu lao wanaweza kuwa wamepotoka na waovu kama Shetani mwenyewe, dhehebu lao linaweza hata kuasi kutoka kwenye ukweli wa Biblia na kubadilisha ukweli huu na na mafundisho ya kuzimu, na bado haitawafanya waone hili! Kwa nini? Kwa sababu wanaamini kwamba dhehebu lao ni Kanisa la kweli la Mungu. Kwa hiyo hata kama wangeonyeshwa ushahidi unaothibitisha kwamba Kanisa lao linatawaliwa na Shetani mwenyewe, isingetikisa imani yao ya upofu katika dhehebu hata kidogo! Hii ni kwa sababu wanaamini kwamba Kanisa lao linasafiri kwenda mbinguni, na kwamba kwa kubaki wameshikamana nalo tiketi yao kwenda mbinguni ndiyo imehakikishwa, lakini kama wangetengwa nalo, wangekuwa wamepotea!

     Ninawaomba na kuwasihi sana kwamba muweze kuona wazi tofauti kubwa kati ya fikra hizi mbili na njia inakuongoza kufuata. Moja inaongoza katika kutofungwa na kitu chochote kabisa na uhuru katika Kristo, na nyingine inaongoza katika kifungo na utumwa kwa wanadamu! Moja ni ukweli wa injili ya Biblia ambayo imejikita kwa Yesu, na nyingine ni udanganyifu wa kutisha wa Ukatoliki ambao unalenga kwa Shetani! Ninatumaini kwa dhati kuwa unaweza kuelewa wazi kwamba ikiwa utaamani kwamba Kanisa la kweli la Mungu ni dhehebu, basi uko katika kifungo cha wanadamu wanaotawala Kanisa hilo. Na, la muhimu zaidi, ni kwamba Kristo ameibiwa kutoka kwanu kama Mwokozi kwa sababu dhehebu limechukua sehemu yake – limekuwa kitu cha ibada yenu na chimbuko la wokovu wenu!

     Mandhari haya ya kusikitisha, ya dhehebu la kikanisa kufanywa kuwa kitu cha ibada badala ya Kristo, ndiyo hasa Wayahudi waliongozwa ndani yake. Na kitu kinachovunja moyo zaidi, ni kwamba wengi wa watu wa dini leo wanaongozwa kuamini kitu kile kile.
     Wayahudi walimshtaki Stefano kwa kutamka “maneno ya makufuru dhidi ya mahali hapa patakatifu” au dhidi ya hekalu (angalia Mdo 6:13). Na maneno ya Stefano yalikuwa ni yapi?
     “Lakini Sulemani alimjengea [Mungu] nyumba. Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii, Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani mtakayonijengea? asema Bwana, Au ni mahali gani nitakapostarehe ? Si mkono wangu uliofanya haya yote.” Mdo 7:47-50.

     Stefano alikuwa kwa msingi anawaeleza washiriki wa Kanisa lote la Kiyahudi kwamba katika kipindi hiki cha Agano Jipya, Mungu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, lakini anahitaji kukaa katika mioyo ya watu binafsi ya watu wake kwa njia ya Yesu kristo. Kwa maneno mengine, Stefano alikuwa anawaambia kwamba yeyote aliyetaka kumwabudu Mungu alipaswa kumwabudu katika roho na kweli, kwamba hakuna yeyote aliyetakiwa kuwa katika dhehebu la Kanisa au kwenda kwenye hekalu lolote  ili apate kumwabudu Mungu. Hii kwa hakika ilimaanisha kwamba hakuna aliyetakiwa kuendelea kushikamana na ukuhani wao uliopotoka tena, lakini angepata pumziko kamili na uhuru wa kudumu kwa Yesu Kristo! Ushuhuda wa Yesu unafanya hili wazi zaidi:
     “Yeye [Stefano] alirejea historia ya hekalu na akatangaza kwamba Mungu hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono. Wayahudi waliabudu hekalu na walijawa na hasira kubwa kwa kitu chochote kilichonenwa kinyume cha jengo hilo kuliko hata kama kingenenwa kinyume na Mungu.” Early Writings, ukr. 198.

     Wayahudi walioabudu hekalu walikuwa na hasira kwamba maneno kama hayo yalinenwa kinyume cha Kanisa lao na mamlaka. Na badala ya kutambua ukweli huu, walipeleka upendo wao na ibada katika hekalu na kuviweka hapo badala ya kuviweka kwa Yesu, walimkataa Kristo, wakakataa ukweli wake, na wakamponda mawe Stefano mpaka kufa. Lakini kitu kinachoshangaza zaidi, ni kwamba katika kipindi hiki cha Agano Jipya, roho hii hii ya uovu, ambayo huinuka kwa dhihaka ya hasira dhidi ya yeyote anayenena kinyume na dhehebu lao, bado inafanya kazi katika mioyo ya wengi leo. Wakati maneno yoyote yanaponenwa ili kuweka wazi maovu na upotofu wa Kanisa lao, au kugusa kwenye mafundisho ya uongo ambayo dhehebu lao linayashikilia, hata kama maneno haya ni ukweli, badala ya kuchunguza kama mada zilizoletwa ni za kweli, huinuka kwa hasira ya dhihaka kinyume na mjumbe na kutaka anyamazishwe mara moja. Hii ni ishara ya ushahidi tu kwamba viongozi wa dhehebu lao wamefanikiwa kumwondoa Kristo katika mioyo yao na kuweka dhehebu mahali pake [Kristo], na wamewaongoza ndugu hawa binafsi kuabudu dhehebu badala ya Mungu pekee. Hebu ndugu hawa binafsi waliodanganywa waamke kabla hawajachelewa, kwa sababu kama hawatabadilisha Kanisa lao la kidhehebu na Yesu Kristo, basi wataongozwa pia kupigana kwa mkono uwao wote wa damu dhidi ya yeyote anayethubutu kusema neno kinyume na sanamu yao-Kanisa, hata mpaka kufikia kuua kama walivyofanya Wayahudi, na bado katika upofu wao wanaamini kwamba wanamtolea Mungu kafara!

     Lakini ndugu, Ukweli wa Biblia ni kwamba hatuko tena chini ya mfumo wa Agano la Kale ambapo uwepo wa Mungu ulikaa katika jumba la hekalu linaloonekana katika Patakatifu pa Patakatifu moja kwa moja juu ya mbao mbili za mawe ambazo Mungu aliandika amri zake 10, na hekalu ambalo iliwabidi watu wakaribie ili wapate kumwabudu. Lakini sisi ni watu wa mfumo wa Agano Jipya, ambapo uwepo wa Mungu unaweza kukaa katika hekalu la miili yetu, ambapo Mungu anahitaji kuandika sheria yake katika mioyo yetu au mawazo!
     “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.” Ebr 8:10.

     “…Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, nitakuwa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” 2 Kor 6:16.

     Kwa hiyo Biblia iko wazi kwamba Kanisa la kweli la Mungu halijajengwa na dhehebu lolote – bila kujali jina lao zuri lililotukuka, bila kujali ni kiasi gani cha ukweli wanachoweza kudai wanaamini au wamepata kufuata kwa miongo kadhaa, bila kujali ni kiasi gani wanatangaza kwa sauti kuwa wamechaguliwa na Mungu, kwa sababu kile kinachojenga Kanisa la Mungu la kweli ni watu binafsi.
     Mungu asifiwe kwa uelewa huu wa ukweli! Sasa watu binafsi hawawezi tena kubaki katika kifungo kwa ukuhani uliopotoka au kwa Kanisa lililopotoka , lakini wanaweza kupata uhuru wa kweli kwa Yesu Kristo! Kwa hiyo, dhehebu lolote au kundi la kidini ambalo linaleta madai kwamba ndilo Kanisa la kweli la Mungu, na hivyo wokovu wako uko hatarini ikiwa utajitenga kwa hiari kutoka kwao, au ukitupwa nje, au ukifutwa ushirika, au kufungiwa kushiriki nao, unaweza kujua basi kwamba wamemtupa Kristo nje ya Kanisa na wamechukua nafasi yake kati ya watu wao! Je, hii ni kweli kwa kiasi gani?

     Biblia hufundisha kuwa ni “kwa njia” tu na “kupitia” kwa Yesu Kristo ndipo tunapata ukweli (Yoh 14:6); kwamba tunakuwa sehemu ya Agano Jipya (2 Kor 3:13-18); kwamba tunapata ukombozi (Rum 3:24; Efe 1:7); kwamba tunahesabiwa haki (Mdo 13:39); kwamba tunakuwa wenye haki (Yer 23:6; 2 Kor 5:21); kwamba tunakuwa na amani na Mungu (Rum 5:1; Flp 4:7; Kol 1:20); kwamba tunaweza kumwendea moja kwa moja Baba (Efe 2:18); kwamba Mungu hutuonyesha wema wake (Efe 2:7); kwamba tunapokea neema (2 Tim 2:1; Efe 2:7); kwamba tunapokea Roho Mtakatifu (Tit 3:6); kwamba tunakuwa wenye hekima (1 Kor 4:10); kwamba tunakuwa hai na tunaishi (Rum 6:11; Flp 1:21; 1 Yoh 4:9; Yoh 14:6); kwamba Mungu hufanya kazi ndani yetu (Ebr 13:21); kwamba tunatakaswa (1 Kor 1:2); kwamba tunafanywa kamili (Kol 1:28); kwamba tunaweza kufanya mambo yote (Flp 4:13); kwamba tunapata ushindi (1 Kor 15:57); kwamba tuna ushindi wa dhambi (2 Kor 2:14); kwamba tunaweza kubaki waaminifu (Efe 1:1); kwamba tunaweza kutunzwa katika utakaso (Yud 1:1); kwamba tunakuwa wana na warithi wa Mungu (Gal 4:7); kwamba tunaweza kufurahia na kushangilia katika Mungu (Rum 5:11, 15:17); kwamba tunapokea mibaraka ya kiroho (Efe 1:3); kwamba tunakuwa matajiri (2 Kor 8:9); na kwamba tunaweza kukaa katika makao ya mbinguni (Efe 2:6)! Hivyo ni katika Yesu na kupitia kwake ndipo tunaweza kujiepusha na laana ya Mungu (Rum 5:9); kwamba tutafufuliwa kama tutakufa kabla Yesu Kristo hajarejea tena (Yoh 11:25); kwamba tunapata wokovu wetu na tutaokolewa (2 Tim 2:10; Yoh 10:9, 3:17); na kwamba tunapata uzima wa milele (2 Tim 1:1; Rum 6:23; 1 Yoh 5:11-12)! Ndiyo maana TUMAINI LETU PEKEE LIMEJENGWA TU KATIKA NA KUPITIA KWA BWANA WETU YESU KRISTO (1 Thes 1:3), kwa sababu kitu chochote na kila kitu kilicho kizuri ndani yetu huja tu kupitia kwake (Flm 6)!
     Yaliyopo hapo juu yanapaswa, pasipo swali na kama hitimisho, kuyakinisha kwa nini msingi wa Kanisa la kweli la Mungu uko kwa Yesu Kristo – Mwamba imara wa milele  (angalia 1 Kor 10:4, 3:11; Zab 62:2, 18:2, 92:15, 2 Sam 22:32)! Hakuna dhehebu, kundi la kidini, viongozi wa dini, ukuhani, mtu au kikundi cha watu, wanaoweza kukupatia vitu viwavyo vyote hapo juu vya ukweli. Mtu pekee anayeweza kukupatia vitu vitu hivi vyote hapo juu katika ukweli, ni Kristo Yesu pekee; siyo Petro, au Papa, au Buddha, au Krishna, au Muhamad, au Maitreya, au mtu yeyote yule – lakini Yesu Kristo peke yake! Kwa hiyo dhehebu lolote au kundi la kidini ambalo linakwambia, au linakuongoza kuamini, kwamba yoyote katika mambo yaliyopo hapo juu yanaweza kupatikana kwa kujiunga na mfumo wao wa kidini, basi unaweza kujua pasipo wasi wasi kwamba ni mawakala waliodanganywa wa Ibilisi, mfumo wao wa Kanisa ni bandia ukikaa kama Kanisa la Mungu, na hivyo ni hila na mtego wa udanganyifu kujaribu na kukuleta wewe jehanamu kwa kumwiba Yesu kutoka kwako kama Mwokozi wako! Ni kwa njia na kupitia kwa Kristo ndiyo tu tunaweza kupata vitu vyote, kuhakikishiwa wokovu wetu na kuwa sehemu ya Kanisa lake la kweli, lakini nje ya Kristo, hatuna chochote, na ni bure!

     Kwa hiyo Kanisa la kweli la Mungu halijajengwa na dhehebu lolote, kwa sababu kile kinachofanya Kanisa la kweli la Mungu ni watu binafsi! Bado ufahamu huu wa kibiblia wa nani na ni ni kinafanya Kanisa la kweli la Mungu hutuongoza sisi kuuliza maswali yafuatayo muhimu: Tufanye nini kila mtu binafsi ili kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu duniani, na jinsi gani tunaweza kuendelea kuwa sehemu yake? Na ni wapi tunaweza kulipata Kanisa hili ili kusudi tuweze kushiriki na ndugu zetu na dada?


Tufanye Nini Kuwa Sehemu ya Kanisa la Kweli Leo?

     Kama tulivyokwisha kujifunza, tunakuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu kwa kuungana na Kristo mwenyewe. Njia pekee ya kushikamana na Kristo ni kwa kutambua kwamba tumevunja sheria ya Mungu na ni wadhambi tunaostahili kifo, na kwamba tunahitaji Mwokozi (1 Yoh 3:4; Rum 3:20, 6:23). Kisha lazima tumkiri Kristo kama Mwokozi wetu binafsi, tutubu na kuungama dhambi zetu, na hatimaye Kristo atatufunika kwa damu yake ya thamani, akitusamehe dhambi zetu tulizotubu na kututakasa na kutuosha sisi kutoka katika mambo yote machafu (1 Yoh 1:7, 9). Yesu hutuhesabia haki bure kutokana na dhambi zetu zote za nyuma kwa njia ya sifa zake za thamani (Rum 3:23-28), hutuvalisha vazi lake la thamani la haki – mavazi haya ya baraka ya wokovu (Isa 61:10), na hutupatia neema yake na nguvu (Rum 5:1-2; Gal 5:1). Hatimaye, tunaweza kusimama mbele ya Baba kikamilifu na haki kamili kana kwamba hatukupata kutenda dhambi kabisa! Tunakuwa wana na binti za Mungu (Rum 8:16; Gal 3:26), tukiwa wana wa nuru na wa mchana (1 Thes 5:5), tukiwa wa pekee na watu watakatifu (1 Pet 2:9) – na hivyo sehemu ya hema ya kweli ya Mungu, hekalu, Kanisa au nyumba (angalia Ufu 21:3; 1 Kor 3:16-17, 6:19; 2 Kor 6:16; Ebr 3:6)!
     Biblia hueleza muujiza huu wa ajabu wa kubadilishwa, kutoka katika kuwa mdhambi kwenda katika mwanaume au mwanamke kamili katika Kristo, kama “kuzaliwa tena” (Yoh 3:3-8; 1 Pet 1:23); kuwa “kiumbe kipya” (2 Kor 5:17; Gal 6:15); “donge jipya” (1 Kor 5:7); “utu mpya” (Efe 4:24; Kol 3:10); “chupa mpya” (Mk 2:21-22; Mt 9:16-17; Lk 5:36-39); n.k. Katika hali hii ya kuhesabiwa haki, kuwa katika “nira” pamoja Kristo (Mt 11:29-30), “tumemvaa” Kristo (Rum 13:14), tuko “ndani” ya Kristo (2 Kor 5:17; Rum 8:1; 1 Pet 5:14), na ni “watumishi wa Mungu” na “wa Kristo” (Rum 6:22; Efe 6:6) – tukiwa watumishi “wa haki” (Rum 6:18-19). Kadiri tunavyoendela kubaki katika hali hii ya kuhesabiwa haki tukiwa “katika” Kristo, na hatuchagui kujitenga sisi wenyewe kutoka kwake, tutaendelea kubaki wasafi na wakamilifu katika Yeye, tukiwa watendaji wa mapenzi yake (Rum 2:13; Yak 1:22), na hivyo tumehakikishiwa wokovu wetu (1 Yoh 5:11-12). Na kadiri ambavyo tunabaki ndani ya Kristo, tunaendelea kuwa sehemu ya Kanisa lake la kweli.
     Lakini kama tungelichagua kujitenga wenyewe kutoka kwa Kristo basi hatuko tena “ndani ya” Kristo, lakini tuko nje. Na ni kitu gani kingesababisha tutengwe kutoka kwa Yesu? Kama tukichagua kuvunja sheria ya Mungu ya amri kumi na hatimaye kutenda dhambi (1 Yoh 3:4), basi mara hiyo hiyo tanatengwa kutoka kwa Mungu na Kristo (angalia Isa 59:1). Kwa kuchagua kutoendelea na kazi ya kusulubisha nafsi (Gal 2:20; Kol 3:1-3), lakini kuchagua kutoa maisha tena kwa mambo ya kimwili ya “utu wa zamani” (Rum 6:6), kwa kuchagua kuongozwa kwa “nia ya mwili” (Rum 8:6-7), basi hatuwezi kusimama tena tukiwa tumehesabiwa haki, wenye haki au wakamilifu mbele za Mungu kwa sababu tumechagua sasa kufanya dhambi na sasa tumenajisiwa na hiyo. Sisi si “viumbe vipya,” au “donge jipya,” au “utu mpya” au “chupa mpya.” Katika hali hii isiyokuwa ya haki hatuendelei kufungiwa “nira” na Kristo, lakini sasa tumefungiwa nira na Ibilisi; “hatujamvaa” tena Kristo, lakini sasa tumemvaa Ibilisi, na si watumishi wa Mungu tena, au wa Kristo, au wa haki, lakini sasa ni watumishi wa Shetani, dhambi, na ubatili (Rum 6:12-13, 19-21)! Hivyo, sisi si sehemu ya Kanisa lake la kweli, na hatuna uhakika zaidi wa wokovu, kwa sababu hatujaendelea kushikamana na Kristo!

     Kama unavyoweza kuona dhahiri, hii ndiyo njia nyembamba na iliyosonga kama ilivyoelezwa juu, lakini hata hivyo ndiyo ukweli wa Biblia (angalia Mt 7:13-14). Tunabaki kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu kwa kuendelea kushikamana na Kristo. Tunaendelea kuungana na Kristo kwa kuchagua kutotenda dhambi. Wale wote wanaochagua kutenda maovu na dhambi hawana uhusiano na Kristo (angalia Lk 13:24-28). Dhambi moja tu inatosha kutuondoa nje ya Kristo, nje ya uhakika wa wokovu, na nje ya kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu!
     Katika ufahamu huu wa ajabu, wengine wanaweza kupinga kwamba pindi tukishamkiri [Yesu] kama Mwokozi wetu binafsi, tunahesabiwa haki milele [tumeokolewa milele], tunaokolewa pale pale, na hivyo haijalishi kuwa ni matendo gani mazuri au mabaya tunaweza kuyafanya baada ya wakati huo kwa sababu tunabaki kuwa watumishi wa Kristo milele! Lakini hiki ndicho Biblia inakifundisha? Hasha.
     “Hamjui kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.” Rum 6:16.

     “Amin, Amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” Yoh 8:34.

     “…maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.” 2 Pet 2:19.

     Kwa hiyo baada ya kumpokea Kristo, kama tukichagua kutenda dhambi, hatuhesabiwi haki katika Kristo, hatuna wokovu tena katika Kristo, sisi siyo tena watumishi wa, au hatuna sehemu yoyote katika Kristo, kwa sababu tumekuwa watumishi wa Shetani. Unaweza tu ukamtumikia Bwana mmoja kwa wakati mmoja, siyo wawili kwa wakati mmoja! Ama unamtumikia Kristo, au unamtumikia Shetani. Kwa hiyo huwezi kuwa mtumishi wa Kristo wakati unapochagua kufanya dhambi!
     “…hakuna mtu anayeweza kutumikia mabwana wawili…” Mt 6:24.

     “Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.” 2 Yoh 9.

     Kama ilivyo kweli hapo juu, hakuna ukweli wa Biblia kuhusiana na imani kwamba ukishampokea Kristo kama Mwokozi wako, basi unahesabiwa haki [katika Yeye] milele kutoka katika dhambi za nyuma, sasa na baadaye! Kuhesabiwa haki ni kwa dhambi tu ambazo umekwishazitenda wakati wa nyuma (angalia Rum 3:24-25). Hivyo, kuhesabiwa haki hakuwezi kutumika kwa dhambi ambazo hazijatendwa, lakini kwa zile tu za nyuma. Kwa hiyo kama ukitenda dhambi, kuhesabiwa kwako haki kwa nyuma hakuwezi kuifunika! Uko katika hali ya kupotea, na unahitajika kutubu dhambi hizi mpya ulizozitenda na kupatanishwa tena na Kristo. Hivyo hakuna walio na hundi ambayo haijajazwa kufunika mwendelezo wao wa dhambi.
     Pia hakuna ukweli wa Kibiblia uwao wote kuhusiana na imani kwamba ukishamkiri Kristo kama Mwokozi wako, basi unaokolewa saa hiyo hiyo. Wakati tunapomkiri Kristo kama Mwokozi wetu, ndiyo tu tumeanza kutembea katika uhusiano wa kuokolewa na Yesu. Wakati huo tunalo tumaini na uhakika wa wokovu, lakini siyo wokovu wenyewe (angalia 1 Thes 5:8; Tit 1:2, 3:7; Kol 1:27; Rum 8:24). Karama ya wokovu, taji isiyoharibika ya uzima wa milele, inatolewa kwako tu mwishoni mwa kipindi chako cha kupimwa imani yako – kama umevumilia, siyo mwanzoni mwa imani yako bila kuwa umevumilia (angalia 1 Pet 1:9; Mt 10:22; Yak 1:12). Wokovu unatolewa kwa wale tu wanaomaliza mashindano ya injili, siyo wale walioanza kukimbia (angalia 1 Kor 9:24-27). Wokovu unatolewa tu kwa wale wanaoshikilia imani ya kweli, siyo wale tu walioanza katika imani (angalia Ufu 3:11). Na wokovu unatolewa tu kwa wale waliovipiga vita vizuri, waliomaliza safari yao, walioitunza imani, siyo wale walioingia vitani hivi karibuni, au ambao ndiyo wameipokea tu imani (angalia 2 Tim 4:7-8). Kwa sababu bado hatujaokolewa, inatupasa kufanya kila linalowezekana, kwa kuendelea na uvumilivu katika kutenda mapenzi ya Mungu, “kutafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele” (Rum 2:7), na kama wengine hawataendelea, basi “watakatiliwa mbali” (Rum 11:22). Hivyo hakuna watu wanaoweza kuendelea kufanya dhambi na bado waamini kwamba watasamehewa!
     Pia hakuna ukweli wa Biblia kuhusiana na imani kwamba mara tu ukimkiri Kristo basi unabaki kuwa mtumishi wake milele. Ama ni mtumishi wa Kristo, ukitenda mapenzi yake ya haki na bila kutenda dhambi, au ni mtumishi wa Shetani, ukitenda matendo yake maovu kwa kufanya dhambi. Hakuna anayeweza kuwatumikia wote wawili Kristo na Shetani kwa wakati mmoja. Hivyo huwezi kuwa mtumishi wa Kristo wakati ukimtumikia Shetani kwa kufanya dhambi!
     Katika Kristo hakuna dhambi (2 Kor 5:21; Yoh 14:30)! Katika Kristo hakuna umoja na Ibilisi, au uovu, au giza na makosa (angalia 2 Kor 6:14-15). Hivyo kama kweli umeshikamana na uko ndani ya Kristo, basi hutakuwa na kuendelea kushikamana na dhambi, au na Ibilisi, au na uovu, au na giza wala kosa. Kwa hiyo kama utachagua kufanya dhambi, unajionyesha wazi wazi kwamba huishi ndani ya, au hujashikamana na, Kristo, na hatimaye unajidhihirisha mwenyewe kuwa si sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu! Kama uko ndani ya Kristo, hutatenda na wala hutendi dhambi, kwa sababu hakuna dhambi ndani yake. Lakini nje ya Kristo hutaweza, na huwezi, kuacha kutenda dhambi! Sasa utakuwa upande gani – ndani ya Kristo au nje yake [kristo]? Huwezi kuwa sehemu zote mbili kwa wakati mmoja!
     “Kila akaaye ndani yake [Kristo] hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao [Kristo – Gal 3:16] wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu…” 1 Yoh 3:6-10.

     Kwa hiyo kama ukitenda dhambi, unajionyesha mwenyewe kuwa hujashikamana na Kristo, lakini ni mwana wa Ibilisi na sehemu ya sinagogi lake la Babeli! Lakini kama, kwa njia ya nguvu na neema ya Kristo (Flp 4:13, 2:12-13; Mk 9:23, 10:27) unapinga dhambi na kamwe hujisalimishi (Yak 4:7-8; Rum 6:11-22), unajionyesha mwenyewe kuwa umeungana na, na umefichwa ndani ya, Kristo na hivyo mwana wa Mungu na sehemu ya Kanisa lake la kweli! Hivyo ni kwa njia ya maneno yako na matendo, au kwa matunda yako, ndipo unapojulikana kuwa ni wa Mungu au wa Shetani!
     “…kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mt 7:17-20.

     Watu wengi, hali kadhalika na madhehebu, kwa sauti wanatangaza kwamba ni sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu, wakati matunda yao yanadhihirisha wazi wazi kuwa wao ni waongo na wafuasi wa Ibilisi! (angalia Ufu 2:9, 3:9; Rum 9:6). Lakini jambo hili linaleta swali jingine: Je, Kanisa la kweli la Mungu laweza kuwa limejengwa na watu wakamilifu pekee wenye haki wanaoishi pasipo kutenda dhambi? Kama ilivyo vigumu kuamini hili, jibu la Kibiblia ni ndiyo!

     Biblia hueleza Kanisa la kweli la Mungu kuwa limejengwa na wale wote walio watakatifu (1 Kor 14:33; Ufu 14:12); wale waliotakaswa (1 Kor 1:2; Yud 1); wale walioimarishwa katika imani na kweli (Mdo 16:5; 1 Tim 3:15); wale walio watii, au wanaojikana nafsi, kwa Kristo (Efe 5:24); wale waliounganishwa kwa Kristo (Efe 5:31-32); na hatimaye wale walio katika Kristo (Gal 1:22; 1 Thes 1:1). Hivyo, Kanisa la kweli la Mungu litakuwa Kanisa la utukufu, lisilo na doa wala kunyanzi au kitu chochote kama hicho (Efe 5:27).
     Wale walio watakatifu hawatendi dhambi. Wale waliotakaswa hawatendi dhambi. Wale walioimarishwa katika imani na ukweli; walio watiifu kwa, au waliojikana nafsi kwa, Yesu; waliounganishwa kwa Kristo, na walio katika Kristo – hawa hawatendi dhambi! Kwa hiyo kama ukichagua kutenda dhambi unaonyesha wazi wazi kwa wengine, hali kadhalika kwako, kwamba wewe siyo mtakatifu, au hujatakaswa, au kukua katika imani na ukweli, au kuwa mtiifu kwa, kuunganishwa kwa, au kuwa ndani ya, Kristo! Hivyo, wewe siyo sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu, na ukiwa nje ya Kristo huna uhakika na wokovu!
     Kwa hiyo Kanisa la kweli la Mungu limejengwa tu na wale wanaoishi maisha makamilifu ya haki bila kuchagua kutenda dhambi, na hii inawezekana kwa njia na kupitia kwa Kristo pekee. Ndiyo maana Kanisa la kweli la Mungu duniani linaweza kuwa moja na Kanisa la mzaliwa wa kwanza wa mbinguni, kwa sababu makundi yote mawili yamejengwa na viumbe wakamilifu wasiotenda dhambi na hivyo huwa katika Kanisa lile lile la kweli la Mungu! (angalia Ebr 12:22-23). Ndiyo maana pia watu wa masalio wanatofautishwa kwa tabia yao, na siyo kwa majigambo yao au jina (Ufu 12:17). “Hakuna jina lolote la dhehebu lina wema wa kutuleta sisi karibu ili tukubalike kwa Mungu” (Review & Herald, Februari 10, 1891), bila kujalisha ni jinsi gani jina hilo limetukuka, kwa sababu Mungu anajihusisha zaidi na tabia yetu! Kama tabia zetu ni sura Mwana wake, tu watoto wa Mungu na sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu. Lakini kama tabia zetu ni sura ya ibilisi, basi tu watoto wa uasi na sehemu ya sinagogi la Shetani la Babeli – bila kujali jina tunalojitambulisha wenyewe!
     “Si kwa jina lake, lakini kwa matunda yake, ndipo tathmini ya thamani ya mti hufanyika. Kama matunda hayafai, jina haliwezi kuokoa mti kutokana na uharibifu. Yohana [mbatizaji] alitamka kwa Wayahudi kwamba kusimama kwao mbele za Mungu kungeamuliwa kwa tabia yao na maisha. Madai tu yasingesaidia. Kama maisha na tabia vilikuwa haviendi sambamba na sheria ya Mungu, hawakuwa watu wake.” Desire of Ages, ukr. 107.

     Kwa hiyo si kwa jina letu, lakini kwa tabia yetu iliyofunuliwa, ndipo tunapojulikana kuwa wa Mungu au wa Shetani. Hivyo, sisi siyo sehemu ya Kanisa la Mungu kama tukichagua kutenda dhambi!
     “Tangu mwanzo, watu walio waaminifu wamefanya Kanisa duniani.” Acts of Apostles, ukr. 11.

     “Hakuna Kanisa jingine mbali na mkusanyiko wa wale walio na neno la Mungu, na wanatakaswa nalo.” Spirit of Prophecy, vol 4, ukr. 237.

     “Wale wanaotunza amri za Mungu, wale wanaoishi si kwa mkate tu, lakini kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, hujenga Kanisa la Mungu aliye hai.” Bible Commentary, vol 7, ukr. 949.

     “Mungu analo Kanisa. Siyo hekalu kubwa, wala siyo [Kanisa] lile lililoimarishwa na Taifa, wala siyo madhehebu mbalimbali; ni watu wanaompenda na kutunza amri zake. ‘Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao’ (Mt. 18:20). Mahali alipo Kristo hata kama ni kati ya wanyenyekevu wachache, hili ndilo Kanisa la Kristo, kwa sababu uwepo wa Mtakatifu aliye juu anayekaa milele zote ndiye tu anayeweza kujenga Kanisa.” Upward Look, ukr. 315.

     Kwa wale ambao wanaweza kujikuta wenyewe katika hali hii ya hatari ya kutokuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu na bila ya uhakika wa wokovu kwa sababu wamechagua kufanya dhambi, hawatakiwi kubaki katika hali hii isiyo na matumaini! Yesu ni Kuhani wenu Mkuu, Mpatanishi na Mkombozi ambaye bado, kwa wakati uliopo, anahudumu katika Patakatifu pa Patakatifu pa Hema ya Mbinguni. Na anawaita ninyi kukimbilia kwake ili kusudi mpate msamaha kamili. Hatamwacha yeyote anayekuja kwa uaminifu kuomba msamaha, lakini kwa rehema atakutakasa, kukuhesabia haki, na kukufanya mwenye haki uliyekamilika ili kusudi upate kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu na upate uhakika wa wokovu ikiwa utabaki kuwa mwaminifu kwake mpaka mwisho!

     Lakini ndugu, kama ambavyo kuna mamlaka mbili tu leo – ama ya Mungu au ya Shetani, kwa hiyo kuna aina mbili za Makanisa leo – ama Kanisa la kweli la Mungu au sinagogi la Shetani la Babeli. Hakuna kuwa sehemu ya katikati, hakuna Kanisa la tatu, hakuna uzio unaoweza kupanda na bado ukapata wokovu. Laodikia ni mchanganyiko wa wema na ubaya ambao hufanya Kanisa lisiwe na Kristo na liwe na muungano na Ibilisi. Kristo kwa hiyo husimama nje ya Kanisa la Kilaodikia, na kubisha mlangoni mwa moyo ili aingie – siyo moyo wa dhehebu, lakini mlango wa moyo wa mtu binafsi.
     “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ufu 3:20.

     “Kanisa liko katika hali ya Laodikia. Uwepo wa Kristo haupo kati yake.” Notebook Leaflets, ukr. 99.

     Wale wanaotenda dhambi hudhihirisha kwamba hawajashikamana na Kristo, na siyo sehemu ya Kanisa lake la kweli tena, hata kama wanaweza kuwa wamemkri Kristo kama Mwokozi wao, na wanaweza kuwa wameishi katika nguvu yake kwa kipindi kirefu cha wakati bila kutenda dhambi! Mungu hana upendeleo kwa watu (Rum 2:11; Kol 3:25; Yak 2:9; 1 Pet 1:17), na wala hapendelei madhehebu au vikundi vya dini kamwe (Mt 23:37-38; Rum 11:12-22). Ikiwa yeyote atachagua kufanya dhambi, haki yao ya maisha yote ya nyuma haiwezi kuwaruhusu kuendelea kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu kwa mwendelezo wa uhakika wa wokovu!
     “Na wewe, mwanadamu, waambie wana wa watu wako, Haki yake mwenye haki haitamwokoa, katika siku ya kukosa kwake...wala yeye aliye mwenye haki hataweza kuishi kwa haki yake, siku ile atakapotenda dhambi. Nimwambiapo mtu mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake aliotenda, atakufa katika uovu huo. Tena, nimwambiapo mtu mwovu, Hakika utakufa; kama akighairi, na kuicha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki…Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi.” Eze 33:12-14, 16.

     “Bwana Yesu atakuwa siku zote na watu waliochaguliwa kumtumikia. Wakati Wayahudi walipomkataa Kristo, Mkuu wa uzima, aliuondoa ufalme wa Mungu kutoka kwao na kuwapatia Mataifa. Mungu ataendelea kufanya kazi katika kanuni hii na kila tawi la kazi yake. Wakati Kanisa linapothibitisha kukosa uaminifu kwa kazi ya Mungu, pasipo kujali nafasi yao waliyomo, bila kujali wito wao wa juu na mtakatifu, Bwana hawezi kuendelea kufanya kazi nao. Hatimaye, wengine huchaguliwa kuchukua majukumu muhimu. Lakini, kama hawa baadaye hawatengenezi maisha yao kwa kuacha kila jambo baya, kama hawatengenezi kanuni safi na takatifu katika mipaka yao yote, basi Bwana atawatweza na kuwanyenyekeza na, wasipotubu, atawaondoa kutoka kwenye sehemu yao na kuwafanya kitu cha aibu.” Upward Look, ukr. 131.

     Hivyo, matunda yako yatadhihirisha wazi leo ni Kanisa gani upo. Kwa hiyo ni Kanisa gani unalionyesha kuwa sehemu yake leo? Ni Kanisa gani unataka kuwa sehemu yake leo? Huu ni wakati hasa wa kuchagua!
     “…Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye.” 1 Fal 18:21.

     “...chaguenii hivi leo mtakayemtumikia…” Yos 24:15.



Ushirika  Pamoja na Kanisa la Kweli la Mungu

     Suala la ushirika na Kanisa la kweli la Mungu limekuwa jambo ambalo limeeleweka vibaya sana. Kutokana na kile ambacho tumejifunza, Kanisa la kweli la Mungu limejengwa na watu walioshikamana wenyewe na Kristo, na siyo dhehebu. Kwa hiyo hakuna dhehebu leo ambalo ni Kanisa la kweli la Mungu. Bado ni mapenzi ya Mungu hasa kwamba watu wake washiriki pamoja kila inapowezekana (angalia Ebr 10:25). Kusema kweli, ni kwa njia ya kushirikiana pamoja ndipo tabia zetu zinajaribiwa, kufunuliwa, na hivyo kuwezeshwa kufikia ukamilifu (angalia Manuscript Releases, vol 11, ukr. 179). Hii inakamilishwa kwa kujifunza kwetu namna ya kuungana pamoja kama kitu kimoja na ndugu zetu na dada, kwa sababu wote hufanya viungo tofauti vya mwili wa Kristo (angalia 1 Kor 12:12-14). Lakini kuna viwango vyovyote vya kuangalia katika kushiriki pamoja, au tuko huru kushiriki na kuabudu pamoja na wale wote wanaojiita wenyewe Wakristo?
     “...bali tukienenda nuruni, kama yeye [Yesu] alivyo katika nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote…” 1 John 1:7.

     Kwa hiyo watu ni lazima washiriki pamoja na wale tu wanaotembea katika nuru kama Kristo alivyo katika nuru. Na kwa sababu katika Kristo hakuna giza au makosa au mafundisho ya uongo kabisa, basi kipimo hiki cha Kibiblia cha ushirika kitawazuia watu wa Mungu kutoabudu na makundi yoyote au Makanisa ambayo yalikuwa hayafuati, kutembea, au kuishi katika kweli yote, lakini yaliyokuwa na mchanganyiko wa ukweli na makosa ndani yake. Hali hii iliyojichanganya, ilileta mchanganyiko wa ukweli na uongo, na hufafanua wazi wazi hali ya madhehebu yote ya leo; yawe ni ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Waadventista, Wale wa Kiroho [Evangelical], Injili Kamilil, Wabudha, Wahindu, Waislamu, Dini ya Mizimu, Occult, n.k. Kwa hiyo makundi yote ya kidini leo hauruhusiwi kushiriki nayo kwa sbabu yote hayatembei katika nuru yote lakini yana mchanganyiko wa ukweli na makosa katika imani zao, na hayako tayari kuacha makosa yao! Na ni mchanganyiko huu wa ukweli na makosa unaoyafanya Makanisa haya yote kuwa sehemu ya Babeli – machafuko!

     Sasa, utafanyaje kama ukijikuta mwenyewe unashiriki tayari katika kundi la kidini ambalo halitembei katika, kuishi sawa na, ukweli wote? Je, utaendelea kushiriki, kuabudu katika, na kubaki kuwa mshiriki wake? Mungu anakwambia HAPANA!
     “Msifungiwe nira na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawa sawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai: kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana mwenyezi.” 2 Kor 6:14-18.

     “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.” Isa 52:11.

     “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu 18:4.

     “Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo….Enyi watu wangu tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.” Yer 51:6, 45.

     Kwa hiyo ni jambo la muhimu kuhusiana na wokovu wetu kwamba tuhakikishe tumejitenga kutoka katika dhehebu lolote lililo na mchanganyiko wa ukweli na makosa ndani yake, au tutawajibika kijumla kwa dhambi zake na tutaangamizwa pamoja na dhehebu hilo. Hivyo, kama ukikataa kuacha madhehebu haya  kama Mungu anavyokuhitaji kufanya, na ukaendelea kushiriki nayo, kuabudu katika, au kubaki mshiriki wake, basi utakuwa sehemu ya Kanisa katika dhambi zake, utapoteza uzima, na utaangamizwa pamoja na Kanisa hilo la Kibabeli – bila kujali Kanisa hilo linajiita jina gani lenyewe, liwe linaitwa “Kanisa Katoliki la Kirumi” au “Kanisa la Mungu” au hata “Waadventista Wasabato!” Ili kuelewa zaidi juu ya mada hii ya uwajibikaji kijumla, tafadhali tuandikie ili upatiwe kijitabu “Kwa Nini Tunawajibika kwa Dhambi za Binafsi, Jamii, na Kijumla?

     Kwa sababu hakuna dhehebu lolote lililoimarishwa leo ambalo linastahili kwetu kushiriki nalo kulingana na vipimo vya neno la Mungu, basi ni wapi tutashiriki pamoja na kumwabudu Mungu? Katika nyumba zetu wenyewe! Mungu hakuiti kujiunga na dhehebu lolote ili upate kumwabudu Yeye leo kwa sababu yote yamenajisiwa na kupotoshwa kwa makosa na dhambi. Lakini Mungu anawaita kweli kumwabudu katika roho na kweli (angalia Yoh 4:20-24), na hili linaweza kukamilishwa kwa urahisi katika nyumba zenu wenyewe – sawa sawa na ilivyokuwa siku za Mitume! (angalia Rum 16:5; 1 Kor 16:19; Mdo 18:7; Kol 4:15; Flm 2.)
     Kama unawajua wengine wanaoamini katika, na wanaotembea na kuishi sawa sawa na, ukweli huu huu wa Kibiblia, na nyote mko karibu sana, basi kulingana na 1 Yohana 1:7 mnaweza na mnatakiwa kushiriki pamoja kila mmoja. Aina hii ya ushirika pamoja na wale tulio wa imani sawa, ambapo kila mmoja anakazana kuwa huru asitende dhambi kwa njia ya Yesu Kristo, inaweza kuwa mbaraka mkubwa na faida kwa sehemu zote zinazohusika – siyo tu kwa kufarijiana sisi kwa sisi, kutiana moyo, na kukua katika maisha ya kiroho na maarifa ya ukweli, lakini kwa kujua kwamba kuna wengine hasa ambao wanapitia mapambano kama mnayopitia, na katika Kristo ni zaidi ya washindi! (angalia Rum 8:37).
     Baadhi ya Makanisa ya nyumbani yanaweza kuwa yana mtu mmoja tu au ya familia moja ambao wanamwabudu Mungu katika roho na kweli. Na kama unamwabudu Mungu peke yako kwa sababu hakuna waumini wengine karibu na wewe, basi ujue kwamba hauko peke yako kabisa, Kwa sababu Baba, Mwana, ushirika wa Roho Mtakatifu, hali kadhalika malaika wako mlinzi wako pale kuunganika na wewe katika ibada (angalia Mt 18:20), na watajaza mahali palipopungua katika kushiriki pamoja kwa kukubariki zaidi! Lakini Makanisa mengine ya nyumbani yanaweza kuwa yamejawa na waumini wakishiriki pamoja. Lakini tafadhali usisahau kwamba Kanisa la kweli la Mungu siyo dhehebu lolote au kundi la kanisa la nyumbani, iwe binafsi au kwa ujumla, kwa sababu Kanisa la kweli la Mungu limejengwa tu na watu binafsi ambao wameshikamana na Kristo na ambao kwa sasa wanaishi maisha makamilifu yasiyo ya dhambi katika Yeye.

     Pia, kama ilivyojidhihirisha katika historia ya nyuma, kadiri kanisa la nyumbani linavyokuwa kubwa, ndivyo Shetani anavyopata mwanya zaidi kuliingilia kupitia kwa mmojawapo wa washiriki wake na hatimaye kusababisha shida ambazo zinatishia wote. Kwa hiyo ili kuzuia hili listokee, Mungu ametoa miongozo maalum kwa wale wanaoshiriki pamoja katika kanisa la nyumbani kufuata na kuendana nazo – na hasa wakati ambapo wanahitaji kushughulikia shida zozote zitakazotokea. Miongozo hii haijapangwa tu kumfungia nje Shetani, bali pia kusaidia kumwokoa kaka au dada aliyeanguka dhambini ili kusudi waendelee kushiriki pamoja nasi. Kwa wale watakaotaka kujua yaliyo mapenzi ya Mungu katika eneo hili muhimu la umoja na jinsi ya kushughulikia shida katikati yetu, tafadhali andika ili kupata kijitabu “JE, UTAJIBU SALA YA BWANA? – Wote Wawe na Umoja.”


     Hebu Mungu atusaidie sisi sote kuelewa kikamilifu suala hili la Kanisa la kweli la Mungu. Hebu na awasaidie ninyi kushikamana na Kristo ili kusudi “mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Pet 2:9). Hivyo wewe, na hali kadhalika ndugu wengine na dada wanaokamilisha Kanisa la kweli la Mungu, muweze kudhihirisha tabia safi ya Mungu na isiyo na doa kwa wengine, kueneza ukweli wa injili yake ya thamani mbali na karibu, na hivyo kujaza ulimwengu huu wa giza kwa nuru yake tukufu ya ukweli (Hab 2:14; Hes 14:21; Ufu 18:1). Na hii yote huanza kwa uchaguzi wako unaoendelea wa kushikamana na kufichwa “katika” Kristo.
     “…Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi (au wanasema wao ni sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu na watu), nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupenda. Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jina jipya.” Ufu 3:8-12.