"LET THERE BE LIGHT" Ministries
SABABU 100 ZA UKWELI WA SUALA LA SABATO
Kwa nini kutunza siku ya Sabato?
Ni nini kusudi la Sabato?
Je, ilifanywa lini, nani aliifanya, na kwa ajili ya nani?
Siku ipi ni Sabato ya kweli?
Wengi hutunza siku ya kwanza ya juma, au Jumapili.
Ni mamlaka gani ya Biblia waliyo nayo kwa kufanya hivyo?
Wengine hutunza siku ya saba, au Jumamosi.
Ni Maandiko gani waliyo nayo kwa kufanya hivyo?
Hapa kuna ukweli kuhusiana na siku zote mbili, kama zilivyoelezwa wazi wazi katika neno la Mungu.
Sababu Sitini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Saba
1. Baada ya kufanya kazi siku sita za kwanza za juma katika kuumba dunia hii, Mungu mkuu alipumzika siku ya saba. Mwanzo 2:1-3.
2. Hii iliweka muhuri [katika] siku hiyo kama siku ya Mungu kupumzika, au siku ya Sabato, kama siku ya Sabato [basi] humaanisha siku ya kupumzika. Kwa kufafanua: Wakati mtu anapozaliwa siku fulani, siku hiyo huwa siku yake ya kuzaliwa. Kwa hiyo wakati Mungu alipopumzika siku ya saba, siku hiyo ilikuwa siku yake ya mapumziko, au siku ya Sabato.
3. Kwa hiyo siku ya saba lazima iwe siku ya Sabato ya Mungu. Je, waweza kubadili siku yako ya kuzaliwa kutoka katika siku uliyozaliwa kwenda katika siku ile ambayo hukuzaliwa? Hasha. Wala huwezi kubadilisha siku ya mapumziko ya Mungu kwenda katika siku ambayo hakupumzika kamwe. Hivyo basi siku ya saba bado ni siku ya Sabato ya Mungu.
4. Mwumbaji aliibariki siku ya saba. Mwanzo 2:3.
5. Aliitakasa siku ya saba. Mwanzo 20:11.
6. Aliifanya siku ya Sabato katika bustani ya Edeni. Mwanzo 2:1-3.
7. Ilifanywa kabla ya kuanguka kwa Adamu; na hivyo basi si kivuli, kwani vivuli havikutolewa mpaka baada ya kuanguka.
8. Yesu alisema kuwa ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu (Marko 2:27); ina maana, kwa ajili ya jamii, kadiri ambavyo neno mwanadamu halijawekewa mipaka, hivyo, kwa Mataifa na hali kadhalika Wayahudi.
9. Ni kumbukumbu ya uumbaji. Mwanzo 20:11, 31:17. Kila wakati tunapopumzika siku ya saba, kama Mungu alivyofanya wakati wa uumbaji, tunaadhimisha tukio kuu.
10. Ilitolewa kwa Adamu, kichwa cha jamii ya wanadamu. Marko 2:27; Mwanzo 2:1-3.
11. Hivyo kupitia kwake [Adamu], kama mwakilishi wetu, na kwenda kwa mataifa yote. Mdo 17:26.
12. Siyo taasisi [fundisho] ya Kiyahudi, kwani ilifanywa miaka 2,300 kabla hata Myahudi kuwepo.
13. Biblia kamwe haiiti Sabato ya Kiyahudi lakini mara zote “Sabato ya Bwana Mungu wako.” Watu wanapaswa kuwa waangalifu namna wanavyoipatia jina lisilofaa siku takatifu ya Mungu ya kupumzika.
14. Rejea zenye ushahidi zinafanywa kuhusiana na Sabato katika kipindi chote cha Wazee wa zamani. Mwanzo 2:1-3, 8:10, 12, 29:27- 28, n.k.
15. Ilikuwa ni sehemu ya sheria ya Mungu kabla ya Sinai. Mwanzo 16:4, 27-29.
16. Kisha Mungu aliiweka katika kiini cha sheria yake takatifu. Mwanzo 20:1-17. Kwa nini aliiweka pale ikiwa isingekuwa kama mausia mengine tisa, ambayo yote yanadhihirisha kuwa hayabadiliki?
17. Sabato ya siku ya saba iliamuriwa na sauti ya Mungu aliye hai. Kumb 4:12-13.
18. Kisha aliiandika amri kwa kidole chake mwenyewe. Mwanzo 31:18.
19. Aliichora katika jiwe linalodumu, ikidhihirisha asili yake ya kutokuharibika. Kumb 5:22.
20. Ilitunzwa kitakatifu katika sanduku [la agano] katika patakatifu pa patakatifu. Kumb 10:1-5.
21. Mungu alikataza kazi siku ya Sabato, hata katika nyakati za kuharakisha sana. Kutoka 34:21.
22. Mungu aliwaangamiza Wayahudi jangwani kwa sababu waliinajisi Sabato. Ezekieli 20:12-13.
23. Ni ishara ya Mungu wa kweli, ambayo kupitia hiyo tunatakiwa kumjua yeye [Mungu] kutoka kwa miungu ya uongo. Ezekieli 20:20.
24. Mungu aliahidi kwamba Yerusalemu ingesimama milele kama Wayahudi wangetunza Sabato. Yeremia 17:24-25.
25. Aliwapeleka utumwani Babeli kwa kuivunja [Sabato]. Nehemia 13:18.
26. Aliuangamiza Yerusalemu kwa kuinajisi [Sabato]. Yeremia 17:27.
27. Mungu ametangaza mbaraka wa pekee kwa Mataifa yote yatakayoitunza [Sabato]. Isaya 56: 6-7.
28. Hii [Sabato] iko katika unabii ambao unarejea kikamilifu katika kipindi cha Ukristo. Isaya 56.
29. Mungu ameahidi kumbariki kila mtu anayetunza Sabato. Isaya 56:2.
30. Bwana anatutaka kuiita “siku yenye heshima.” Isaya 58:13. Jihadhalini sana, enyi mnaofurahia kuiita “Sabato ya Kiyahudi ya zamani,” “nira ya kifungo,” n.k..
31. Baada ya Sabato takatifu kuwa imekanyagwa chini kwa “vizazi vingi,” itarejeshwa katika siku za mwisho. Isaya 58:12-13.
32. Manabii wote watakatifu waliitunza siku ya saba.
33. Wakati Mwana wa Mungu alipokuja, aliitunza siku ya saba maisha yake yote. Luka 4:16; Yohana 15:10. Hivyo, alifuata kielelezo cha Baba yake wakati wa uumbaji. Je, hatutakuwa salama kwa kufuata kielelezo cha Baba na Mwana?
34. Siku ya saba ni siku ya Bwana. Angalia Ufunuo 1:10; Marko 2:28; Isaya 58:13; Kutoka 20:10.
35. Yesu alikuwa Bwana wa Sabato (Marko 2:28); hii ina maana [kuwa], kuipenda na kuitunza, kama mume alivyo bwana wa mwanamke, kumpenda na kumthamini. 1 Petro 3:6.
36. Aliitetea Sabato kama amri ya rehema iliyopagwa kwa ajili ya mema ya mwanadamu. Marko 2:23-28.
37. Badala ya kuitangua Sabato, kwa uangalifu alifundisha namna ilivyotakiwa kutunzwa. Mathayo 12:1-13.
38. Aliwafundisha mitume wake kwamba hawatakiwi kufanya lolote siku ya Sabato lakini kilichoamuriwa “kisheria.” Mathayo 12:12.
39. Aliwaelekeza mitume wake kwamba Sabato kwa maombi ilipaswa kuangaliwa miaka 40 baada ya ufufuo wake. Mathayo 24:20 (kukimbia kwao kulitokea mwaka 66 BK).
40. Wanawake watauwa waliokuwa wamekaa pamoja na Yesu kwa uangaifu walitunza siku ya saba baada ya kifo chake. Luka 23:56.
41. Miaka thelathini baada ya ufufuo wa Kristo, Roho Mtakatifu kwa wazi anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 13:14.
42. Paulo, mtume kwa Mataifa, aliita “siku ya Sabato” mwaka 45 BK. Mdo 13:27. Je, Paulo hakujua? Au tuwaamini walimu wa kisaa, wanaodai kwamba ilikoma kuwa Sabato wakati wa ufufuo wa Kristo?
43. Luka, mwanahistoria wa Kikristo aliyevuviwa, akiandika baadaye mwaka 62 BK, anaiita “sikuya Sabato.” Mdo 13:44.
44. Waongofu Mataifa waliita Sabato. Mdo 13:42.
45. Katika Baraza kuu la Kikristo, mwaka 52 BK, mbele ya mitume na maelfu ya wafuasi, Yakobo anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 15:21.
46. Ilikuwa ni desturi kuwa na mikutano ya maombi katika siku hiyo. Mdo 16:13.
47. Paulo alisoma maandiko katika mikutano ya hadhara katika siku hiyo. Mdo 17:2-3.
48. Yalikuwa ni mazoea yake kuhubiri katika siku hiyo. Mdo 17:2.
49. Kitabu cha Matendo ya Mitume hutupatia kumbukumbu ya yeye kuendesha mikutano themanini na nne katika siku hiyo. Angalia Mdo 13:4, 44, 16:13, 17:2, 18:4, 11.
50. Hayakuwepo mashtaka yoyote baina ya Wakristo na Wayahudi kuhusiana na siku a Sabato. Huu ni uthibitisho kwamba Wakristo bado waliitunza siku ile ile ambayo Wayahudi waliitunza.
51. Katika mashtaka yao yote dhidi ya Paulo, hawakumshtaki kwa kuiacha siku ya Sabato. Kwa nini hawakufanya hivyo kama hakuitunza?
52. Paulo mwenyewe alitangaza wazi wazi kwamba alikuwa ameitunza sheria. “Mimi sikukosa neno juu ya sheria ya Wayahudi, wala juu ya hekalu, wala juu ya Kaisari.” Mdo 25:8. Je, ni namna gani hii ingekuwa kweli kama angekuwa hajatunza Sabato?
53. Sabato inatajwa katika Agano Jipya mara 59, na mara zote ni kwa heshima, ikibeba heshima iliyokuwa nayo katika Agano la Kale, “siku ya Sabato.”
54. Hakuna neno lililosemwa katika Agano Jipya kuhusu Sabato kuondolewa, kutanguliwa, kubadilishwa, au kitu chochote cha aina hiyo.
55. Mungu alikuwa hajapata kutoa ruhusa kwa mtu yeyote kufanya kazi katika siku hiyo. Msomaji, ni kwa mamlaka gani unatumia siku ya saba kwa kazi za kawaida?
56. HakunaMkristo wa Agano Jipya, ama kabla au baada ya ufufuo, aliyepata kufanya kazi ya kawaida siku ya saba. Tafuta mfano wa kitu kimoja tu cha aina hiyo, na tutalisalimisha suala zima. Kwa nini Wakristo wa kisasa wafanye tofauti kutoka kwa Wakristo wa Biblia?
57. Hakuna kumbukumbu kwamba Mungu alipata kuondoa mbaraka wake au utakaso kutoka siku ya saba.
58. Kama tu Sabato ilivyotunzwa katika Edeni kabla ya kuangka, ndivyo itakavyotunzwa milele katika nchi mpya baada ya ukombozi. Isaya 66:22-23.
59. Sabato ya siku ya saba ilikuwa ni sehemu ya sheria ya Mungu, kulingana na ilivyotoka katika kinywa chake mwenyewe, na ikaandikwa kwa kidole chake mwenyewe juu ya jiwe katika Sinai. Angalia Kutoka 20. Wakati Yesu alipoanza kazi yake, alitangaza wazi wazi kwamba hakuja kuitangua torati. “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii.” Mathayo 5:17.
60. Yesu kwa ukali aliwashutumu Mafarisayo kama wanafiki kwa kujifanya kumpenda Mungu, na wakati huo huo waliitangua moja ya Amri Kumi kwa mapokeo yao. Katika njia ile ile, kutunza Jumapili ni kubatilisha sheria ya Mungu na ni mapokeo ya wanadamu.
Tumetoa sasa sababu za wazi 60 kutoka katika Biblia kuhusiana na ukweli wa siku ya Saba. Je, utazifanyia nini?
Sababu Arobaini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Kwanza ya Juma
1. Kitu cha kwanza kabisa kilichowekwa kwenye kumbukumbu za Biblia ni kazi iliyofanywa siku ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Mwanzo 1:1-5. Hii ilifanywa na Mwumbaji mwenyewe. Ikiwa Mungu aliumba dunia siku ya Jumapili, je itakuwa ni vibaya kwetu kufanya kazi siku ya Jumapili?
2. Mungu anawaamuru watu kufanya kazi siku ya kwanza ya juma. Kutoka 20:8-11. Je, ni makoa kumtii Mungu?
3. Hakuna hata mzee wa zamani aliyepata kuitunza.
4. Hakuna hata manabii watakatifu waliopata kuitunza.
5. Kwa amri iliyofafanuliwa ya Mungu, watu wake watakatifu walitumia siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kufanya kazi kwa miaka 4,000, angalao.
6. Mungu mwenyewe huiita “siku ya” kufanya kazi. Ezekieli 46:1.
7. Mungu hakupumzika katika siku hii.
8. Hakuibariki kamwe.
9. Kristo hakupumzika katika siku hii.
10. Yesu alikuwa seremala (Marko 6:3) na akafanya shughuli hiyo mpaka alipokuwa na miaka 30. Aliitunza Sabato na kufanya kazi kwa siku sita katika juma, kama wote wanavyokiri. Hivyo basi alifanya kazi nyingi ngumu za siku ya Jumapili.
11. Mitume walifanya kazi katika siku hii wakati wa kipindi hiki hiki.
12. Mitume kamwe hawakupumzika katika siku hiyo.
13. Kristo kamwe hakuibariki.
14. Haijapata kubarikiwa kwa mamlaka yoyote ya Mungu.
15. Haijapata kutakaswa kamwe.
16. Hakuna sheria iliyopata kutolewa kulazimisha kuitunza [Jumapili], hivyo basi hakuna dhambi kufanya kazi katika siku hiyo. “Maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Warumi 4:15; (1 Yohana 3:4).
17. Hakuna mahali popote ambapo Agano Jipya hukataza kazi kufanyika siku ya Jumapili.
18. Hakuna adhabu inayotolewa kwa kuivunja.
19. Hakuna mbaraka unaoahidiwa kwa kuitunza.
20. Hakuna maelekezo yaliyotolewa juu ya namna inavyopaswa kutunzwa. Je, hii ingekuwa hivyo kama Bwana alitutaka kuitunza?
21. Haiitwi kamwe Sabato ya Kikristo.
22. Haiitwi kamwe siku ya Sabato kabisa.
23. Haiitwi kamwe siku ya Bwana.
24. Haiitwi kamwe hata siku ya mapumziko.
25. Hakuna heshma yoyote takatifu inatumika juu yake. Ikiwa ni hivyo basi ni kwa nini tuiite takatifu?
26. Inaitwa tu kirahisi “siku ya kwanza ya juma.”
27. Yesu kamwe hajataja katika njia yoyote--hakuweka jina lake kinywani mwake kulingana na kumbukumbu zinavyoonyesha.
28. Neno Jumapili kamwe halionekani katika Biblia kabisa.
29. Wala Mungu, Kristo, hata watu waliovuviwa, waliopata kusema neno moja kuipendelea Jumapili kama siku takatifu.
30. Siku ya kwanza ya juma imetajwa mara nane tu katika Agano Jipya lote. Mathayo 28:1; Marko 16:2, 9; Luka 24:1; Yohana 20:1, 19; Mdo 20:7; 1 Wakorintho 16:2.
31. Kati ya haya, ni mafungu sita yanayorejea katika siku ile ile ya kwanza ya juma.
32. Paulo aliwaelekeza watakatifu kuangalia mambo yao ya kidunia katika siku hiyo. Wakorintho 16:2.
33. Katika Agano Jipya lote tuna kumbukumbu ya mkutano mmoja tu wa kidini ulioendeshwa katika siku hiyo. Mdo 20:5-12.
34. Hakuna siri kwamba walikuwa na mkutano siku hiyo kabla au baada yake.
35. Haikuwa desturi yao kukutana katika siku hiyo.
36. Hakukuwa na umuhimu wa kumega mkate katika siku hiyo.
37. Tuna kumbukumbu tu ya tukio moja ambamo ulifanyika. Mdo 20:7.
38. Huo ulifanyka usiku--baada ya usiku wa manane. Mistari ya 7-11. Yesu aliisherehekea siku ya Alhamisi jioni (Luka 22), na mitume mara nyingine walifanya hilo kila siku. Mdo 2:42-46.
39. Biblia kamwe haisemi popote kwamba siku ya kwanza ya juma huadhimisha ufufuo wa Kristo. Haya ni mapokeo ya wanadamu, ambayo huifanya sheria ya Mungu kuwa bure. Mathayo 15:1-9. Ubatizo huadhimisha mazishi na ufufuo wa Yesu. Warumi 6:3-5.
40. Mwishoi, agano Jipya liko kimya kwa ujumla kuhusiana na badiliko lolote la siku ya saba kama siku ya Sabato ya Mungu au utakatifu wowote uliotolewa kwa Jumapili – siku ya kwanza.
Kwa hiyo baada ya kupitia sababu hizi za ukweli wa Biblia juu ya suala hili, zikionyesha kwa kuhitimisha kwamba siku ya saba ya juma, au Jumamosi, ni Sabato ya Bwana ktika Agano la Kale na Jipya, ni nini unapaswa kuwa mwitikio wetu kwa amri hii ya nne ya Mungu?
“Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote….Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyengia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” Waebrania 4:4, 9-11.
“Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake....Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.” 1 Yohana 2:3-5, 5:2-3.
“Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Ufunuo 22:14-15.
“Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14.
Kwa kupata habari zaidi juu ya mada hii muhimu, tafadhali bonyeza hapa
|
||